Skip to main content
Skip to main content

Wagonjwa wa selimundu wanasikitikia gharama ya juu ya matibabu

  • | Citizen TV
    52 views
    Wagonjwa wa selimundu pamoja na wazazi wenye watoto walioathirika kaunti ya Busia wamesikitikia kupanda kwa gharama za matibabu. Wamesikitika kuwa wengi wao wameshindwa kumudu bei ya juu ya dawa za kila siku na vipimo vya mara kwa mara vya damu mbali na uangalizi wa kitaalamu. Wagonjwa wanasema wamelazimika kusalia nyumbani bila matibabu. Wameihimiza serikali kupunguza bei ya dawa hizo na kuhakikisha kuwa zinapatikana kwa urahisi, kwani baadhi wamepata ulemavu kwa kukosa matibabu. Ukosefu wa damu hospitalini pamoja na uhaba wa madaktari wataalam wa damu mashinani hulazimu wagonjwa kusafiri mbali na kutumia fedha nyingi kupata matibabu.