Wahamiaji kutoka ‘Afrika na Kote Ulimwenguni’ Wanakusanyika Kati ya Vizuizi vya Mpakani Marekani

  • | VOA Swahili
    571 views
    Mamia ya wahamiaji wamekusanyika kati ya vizuizi viwili vya  mpaka wa Marekani na Mexico karibu na San Diego, California, wakisubiri kushughulikiwa na idara ya Forodha na Ulinzi wa Mpakani ya Marekani. Wafanyakazi wa misaada wamesema wahamiaji hao walitokea maeneo mbali mbali hadi huko Afrika Magharibi, Amerika ya Kati na Asia. Hassan Hamza kutoka Ghana ambaye amekuwa akisafiri kwa wiki sita, anasema: “Si rahisi. Tulianzia kutoka Brazil kwa njia ya barabara. Si rahisi. Watu wa Mexico, wametupa wakati mgumu sana. Si  rahisi, bwana. Si rahisi. Afrika ni gumu kwetu sisi, ndiyo maana tunakimbia kutafuta faraja, unajua hilo. Kwa hiyo mimi na ndugu zangu wa kiume hawa, tunatokea Afrika na tumefika hapa kwa rehema ya mwenyenzi mungu. Marekani ni nchi yenye fursa nyingi. Tuko  hapa ili tuweze kuwa na maisha mazuri. Tunakimbia ukandamizaji unaotukabili. – Reuters #migrants #border #usborder #sandiego #ghana #africa #voa