Wahifadhi wa misitu kutoka eneo la Sabaki walalamikia uharibifu wa maeneo ambayo yamehifadhiwa

  • | Citizen TV
    302 views

    Wahifadhi wa misitu kutoka eneo la sabaki kaunti ndogo ya magarini kaunti ya kilifi wanalalamikia uharibifu wa maeneo ambayo yamehifadhiwa hasa katika misitu ya mikoko. Wakizungumza na wanahabari, wahifadhi hao wa misitu wanasema kuwa wanyakuzi wa ardhi wamenyakua mashamba ambayo yamekua yakihifadhi miti ya mikoko na kuwa hali hiyo itahatarisha juhudi zao za kuboresha misitu kaunti hiyo.