Wahudumu Wa Afya Kaunti Ya Busia Waanza Mgomo

  • | Citizen TV
    274 views

    Maafisa wa utibabu katika kaunti ya Busia wameanza mgomo wao rasmi usiku wa leo na kusitisha huduma za afya katika kaunti hiyo.Maafisa hawa wanawania kushinikiza serikali ya Busia kutekeleza matakwa yao ya kuongezewa na kuwalipa mishahara kwa wakati mwafaka, kuwapandisha vyeo pamoja na kuwaongeza marupurupu. Wahudumu hawa wamesema kuwa wamesitisha huduma za afya hadi maslahi yao yasikizwe.