Wahudumu wa afya wajiandaa kugoma kaunti ya Busia

  • | Citizen TV
    172 views

    Wanachama wa muungano wa wauguzi na maafisa wa kliniki katika kaunti ya Busia watasitisha kutoa huduma hapo kesho. Hii ni kutokana na taarifa kuwa serikali ya kaunti imefeli kuwasilisha makato ya mishahara yao kwa NSSF, NHIF na kwa benki kulipia mikopo yao licha ya kukatwa fedha hizo kutoka kwa mishahara.