Wahudumu wa afya wasitisha mgomo kaunti ya Machakos

  • | Citizen TV
    559 views

    Wahudumu wa afya katika kaunti ya Machakos wamesitisha mgomo uliopangwa kufanyika baada ya gavana Wavinya Ndeti kuahidi kushughulikia lalama zao.Wavinya alisema kuwa ifikapo tarehe 27 mwezi huu kila mhudumu atapata barua zake za kupandishwa cheo huku akiongeza kuwa wataweka kamati za kufanya kazi kuanzia ngazi ya 5, 4 hadi zahanati. Aidha, gavana alitoa wito kwa madaktari kuwahudumia wagonjwa kwa njia ifaayo ili kuboresha hali ya afya nchini.