Wahudumu wa Afya watoa ilani ya kugoma katika kaunti ya Machakos

  • | Citizen TV
    60 views

    Wahudumu wa Afya kaunti ya Machakos wametoa ilani ya mgomo kwa serikali ya kaunti wakilalamikia miongoni mwa mambo mengine kupandishwa vyeo. Wahudumu hao wanaojumuisha wale wa chama cha Madaktari cha KMPDU, chama cha kitaifa cha Wauguzi na muungano wa kitaifa wa Maafisa Kliniki wamesema kuwa mikutano waliyokuwa wakifanya na serikali ya kaunti haijazaa matunda. Wakiongozwa na mwenyekiti wa KMPDU, tawi la Mashariki ya Chini, Charles Okumu wameshikilia haja ya maslahi yao kushughulikiwa kwa haraka, la sivyo, watagoma katika muda wa siku 7 zijazo.