Wahudumu wa bodaboda watakiwa kuwa waangalifu ili kupunguza visa vya kutapeliwa kaunti ya Nandi

  • | Citizen TV
    299 views

    Wahudumu wa bodaboda kaunti ya Nandi wametakiwa kuwa waangalifu zaidi ili kupunguza visa vya baadhi yao kutapeliwa na watu wanaojifanya maafisa wa kukusanya pikipki zilizoshindwa kulipia mikopo. Haya yanajiri baada ya wahudumu wa bodaboda kulalamika kuhusu kuhangaishwa na kampuni zinazotoa huduma zinazowawezesha wenyeji kupata pikipiki kwa mikopo. Kulingana na viongozi wa wahudumu hao ,maafisa wa mikopo wanapaswa kuwasiliana na kushirikiana na viongozi wa wahudumu wa bodaboda kabla ya kukusanya pikipiki.