Waindonesia 'Wakitubia mwezi wa Ramadhan kwa kuondoa tattoo

  • | VOA Swahili
    174 views
    Programu ya kuondoa tattoo iliyosimamiwa na shirika la Amil Zakat National Agency (BAZNAS), jumuiya ya msaada ya Kiislam ya Indonesia imetoa huduma hiyo bila ya malipo, wakati wa mwezi mtukufu wa Waislam wa Ramadhan. Zaidi ya Waindonesia mia moja waliokuwa na michoro ya tattoo, baadhi yenye maua na wengine mkono ukiwa umejaa nyoka na chui, walijiandikisha kupitia mchakato wenye shida na uchovu mwaka huu, wengine ikibidi warejee mara kadhaa kukamilisha kuondolewa tattoo. Raja Zamzami, mratibu wa programu hiyo ikiwa ni mwaka wa nne kufanyika, alisema kuondoa tattoo unamuwezesha Muislam fursa ya "kutubia". #tattoo #amilzakatnationalagency #jumuiya #vijana #waislam #nyoka #chui #uislam #indonesia #jakarta #rajazamzami #voa #voaswahili