Wakaazi Biafra walalamikia kukosa stima kwa miezi mitatu

  • | Citizen TV
    1,698 views

    Wakaazi wa mtaa wa Biafra katika mtaa wa Eastleigh hapa Nairobi wanalalamikia kutokuwa na huduma za umeme kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Wakaazi hao wanasema wafanyikazi wa kampuni ya Kenya Power waliondoa transfoma kutoka eneo hilo tangu mwezi Juni, na sasa wanalalamikia kuathirika kwa huduma za matibabu, biashara na hata utovu wa usalama.