Wakaazi wa Busia watetea hazina ya NG-CDF

  • | Citizen TV
    89 views

    Huku shughuli ya kukusanya maoni ya wakenya kuhusiana na kuhalalishwa kwa hazina za NGCDF, NGAAF na ile ya utendakazi wa maseneta zikitarajiwa kukamilika hii leo, wakazi kutoka maeneo mbalimbali ya kaunti ya Busia wanazidi kujitokeza ili kunakili maoni yao. Katika eneo bunge la Teso Kaskazini, mamia ya wakazi wakiwemo wanafunzi wa shule za upili na wale wa vyuo vya kadri walionufaika na hazina hizo wamejitokeza ili kushuhudia matukio hayo.