Wakaazi wa Kajiado wafunga barabara ya Rombo wakilalamikia ubovu wake

  • | Citizen TV
    501 views

    Shuguli za uchukuzi na biashara zimetatizika pakubwa katika mji wa Rombo kaunti ya Kajiado baada ya wakazi waliokuwa na ghadhabu kufunga barabara hiyo wakilalamikia ubovu wake.Wakazi hao wanalalama kuwa licha ya kulalamika kila mara barabara hiyo inayounganisha Kajiado na Taita Tavet, hakuna hatua ambazo zinachukuliwa. wakazi hao ambao ni wakulima wamekosa kufikisha mazao yao sokoni.Tuungane naye Robert Masai ambaye yuko kwenye maandamanao hayo.