- 503 viewsDuration: 1:59Shughuli za usafiri zilitatizwa jana jioni kwenye barabara ya Chavakali kwenda Kapsabet baada ya wanainchi wenye hamaki kufunga barabara hiyo eneo la Kaptik eneo bunge la Hamisi kaunti ya Vihiga kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi wawili wa shule ya upili ya Kaptik na mhudumu wa bodaboda . Watatu hao ni wasichana wawili na muhudumu wa boda boda huku mwanafunzi mmoja akiendelea kupokea matibabu katika hospitali moja kaunti ya nandi . Wakazi wakilalamikia hali mbaya ya barabara hiyo wakilaumu mwanakandarasi anayejenga barabara hiyo.