Wakaazi wa Kasemeni, Kinango walalamikia bwawa kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    148 views

    Wakaazi wa Kasemeni eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wametaka serikali kuu kusitisha mradi wa ujenzi wa bwawa la Mwache hadi pale wale walioathirika na mradi huo watakapolipwa fidia. Wakaazi hao wanadai zaidi ya familia 900 bado hazijalipiwa fidia ya huku zaidi ya shillingi bilioni 1.9 zikiwa hazijalipwa wenyeji walioathirika. Ujenzi wa bwawa hilo unaogharimu shilingi bilioni 18 ukiendelea wakaazi kutoka vijiji 19 wanasema unafaa usimamishwe hadi pale makubaliano yote baina yao na serikali yatatimizwa.