Wakaazi wa Kilifi waanza juhudi za kupanda miti kwa wingi

  • | Citizen TV
    Serikali ya kaunti ya Kilifi sasa inazitaka shule zote na taasisi mbali eneo hilo kupanda miti Zaidi ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo. Katika taarifa kwa wanahabari baada ya kupanda miti katika shule ya upili ya wasichana ya Kadzonzo kule Mariakani kaunti ya Kilifi waziri wa mazingira eneo hilo Kiringi Mwachitu alisisitiza haja ya upanzi wa miti eneo hilo ili kuongeza msitu kutoka asilimia 7.6 hivi sasa hadi 10 na hata Zaidi