- 664 viewsDuration: 2:06Wakaazi wa Kisimani na ziwa la Ngombe huko Mombasa walifanya maandamano ya amani kulalamikia kukamatwa kwa mzee wa mtaa wa eneo hilo kwa madai ya kuhusika na dawa za kulevya. Kulingana na wakazi mzee huyo amekuwa nguzo kuu ya kuhimiza kuboreshwa kwa usalama katika eneo hilo na kukamatwa kwake kumechangiwa na wanaopinga juhudi za kukabiliana na magenge ya wahuni. Waandamanaji hao walielekea hadi barabara kuu ya Mombasa-Malindi na kusababisha msomgamano wa magari. Aidha wameapa kuendelea na maandamano hadi pale kiongozi huyo atakapoachiliwa huru.