Skip to main content
Skip to main content

Wakaazi wa Magarini wamefanya maandamano ya amani kupinga unyakuzi wa eneo la umma ufuoni

  • | Citizen TV
    58 views
    Wakaazi wa eneo la Mjanaheri kaunti ndogo ya Magarini wamefanya maandamano ya amani wakipinga madai ya mpango wa mwekezaji kunyakua ufuo wa umma. Wakiwa wamebeba mabango, wakazi hao walimshutumu mwekezaji huyo kwa hatua hiyo. Kulingana na wakazi hao eneo hilo ni la umma na lkivutio kutokana na mchanga wake wa kipekee katika ufuo wa bahari hindi. Eneo hilo linajulikana kama Dubai Ndogo na linazidi kupata umaarufu kwa kuwa kivutio kikubwa cha utalii. Wakaazi hao walisema kuwekewa uzio eneo hilo kutawazuia wananchi kupata ufuo huo na kuapa kutokubali hatua hiyo.