Wakaazi wa kaunti ya marsabit wanakumbana na changamoto kutokana na ubovu wa barabara huku maeneo ya Manyatta otte, Manyatta Gidha, Nyayo ,Shauri yako,Songa pamoja na Shurr yakiathirika zaidi.
Aidha shughuli za usafirishaji wa bidhaa hadi sokoni katika maeneo bunge ya North Horr na Laisamis ni baadhi za maeneo zimetatizika pakubwa huku abiria na madereva wakilazimika kukatiza shughuli zao mara kwa mara. Mamia ya Wakaazi Katika kijiji cha manyatta Gindha eneo bunge la Saku wamelalamikia kutelekezwa kwa muda mrefu na serikali ya kaunti na ile ya kitaifa.