Wakaazi waandamana kupinga kuanzishwa kwa mradi wa uchimbaji madini eneo la Ganze, Kilifi

  • | Citizen TV
    192 views

    Wakaazi wa kijiji cha Nyari eneo la Ganze, kaunti ya Kilifi, wameandamana wakipinga kuanzishwa kwa mradi wa uchimbaji madini ya Titanium eneo hilo na mwekezaji mmoja kutoka Uchina. Kulingana na wakaazi hao, tayari wameiandikia barua wizara ya madini kusitisha utoaji wa leseni ya mradi huo, wakidai kuwa hawajahusishwa vilivyo na wala hawajakabidhiwa ripoti ya mazingira kuhusu athari za mradi huo. wakaazi wanahofia kupoteza ardhi zao kwani tayari mwekezaji huyo anakamilisha hatua za kutafuta leseni ya kuanza uchimbaji madini eneo hilo.