Wakaazi waliobomolewa makazi yao eneo la Diani na Tiwi miaka mitatu iliopita wadai fidia

  • | Citizen TV
    203 views

    Wakaazi wa shamba la Cheteni Debwe katika maeneo ya Diani na Tiwi kaunti ya Kwale waliobomolewa makazi yao miaka mitatu iliopita wanataka kulipwa fidia ya hasara waliopata baada ya kuwachwa bila makao. Wakaazi hao wanadai mwekezaji aliyewabomolea makaazi yao akidai umiliki wa ardhi hiyo ya ekari 1000 haitumii huku wao wakiendelea kuhaingaika. Wanadai ardhi hiyo ilimaliza kukodishwa mwaka wa 2013 baada ya makubaliano ya mwaka wa 1914 na ilipaswa kuregeshewa wananchi kupitia serikali ya mtaa.