Wakandarasi waonywa dhidi ya kutokamilisha miradi Narok

  • | Citizen TV
    473 views

    Mratibu wa bonde la Ufa Maalim Mohammed amehimiza wanakandarasi kuhakikisha kuwa wanamaliza miradi ya serikali chini ya muda wa maelewano. Mohammed ambaye pia ni mwenyekiti wa miradi ya maendeleo aliyasema haya alipozuru na kukagua miradi mitatu mikuu ya serikali mjini Narok na viungani mwake. Kati ya miradi aliyokagua ni pamoja na daraja lililoko enea la Jela ya Narok ,barabara mpya ya polong'a,kiwanda cha ngozi cha Euasonyiro na barabara ya itakayoelekea katika ofisi za kamishna wa Kaunti hiyo.