Wakati Russia ikizidisha mashambulizi, Marekani yatoa msaada mpya kwa Ukraine

  • | VOA Swahili
    11,151 views
    - Russia inapoendelea kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, Rais wa Marekani analiomba Bunge la Marekani Alhamisi kuidhinisha msaada mpya kwa ajili ya Jeshi la Ukraine. - Ukraine imesema kwamba mashambulizi ya Russia mashariki mwa nchi hiyo yameongezeka sana, huku miji kadhaa ikishambuliwa katika jaribio la wanajeshi wa Russia kutaka kuwazingira wanajeshi wa Ukraine. -Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema Marekani itatoa msaada wa zaidi ya dola milioni 200 kwa Pembe ya Afrika. Msaada huo utajikita katika kushughulikia mahitaji ya kibinadamu yanayosababishwa na ukame na mzozo wa kikanda. - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.