Wakazi katika kaunti ya Kwale wataka kituo cha Polisi Mwaroni kuhifadhiwa na serikali

  • | Citizen TV
    160 views

    Wakaazi wa Diani kaunti ya Kwale wanataka kuhifadhiwa na kuratibiwa kama turathi ya kitaifa Kituo cha kwanza cha polisi mjini humo kilichojengwa wakati wa ukoloni katika kijiji cha Mwaroni wadi ya Gombato. Majengo yake yaliyoko kwenye ardhi ya tariban ekari nne yanaendelea kuporomoka wenyeji wakihofia huenda historia ya kituo hicho ikaangamia.