Skip to main content
Skip to main content

Wakazi Kirinyaga walazimisha viongozi kufungua madarasa Kadawa

  • | Citizen TV
    221 views
    Duration: 2:38
    Kizaazaa kimeshuhudiwa kijijini Kadawa, eneo la Murinduko, Kaunti ya Kirinyaga, baada ya wakazi wa eneo hilo kuwalazimisha wabunge wawili kutoka kaunti hiyo kuyafungua madarasa matano ya Shule ya Msingi ya Kadawa. Wakazi hao walilalamikia kuchelewa kuzinduliwa kwa ufunguzi wa madarasa hayo miezi miwili baada ya ujenzi kukamilika. Wakazi walisitisha kikao hicho kilichokuwa kikihudhuriwa na Mwakilishi wa Kike Njeri Maina na Seneta Kamau Murango.