Wakazi Laikipia waandamana kudai haki ya Julia Njoki

  • | Citizen TV
    4,061 views

    Shughuli zilisitishwa mchana kutwa mjini Nanyuki kaunti ya Laikipia baada ya maafisa wa usalama kukabiliana na vijana waliojitokeza barabarani kudai haki kufuatia kifo cha Julia Wangui Njoki mikononi mwa maafisa gereza. Mji huo uligeuzwa uwanja wa makabiliano huku polisi wakirusha vitoa machozi kuwatawanya wakaazi. Haya yamejiri huku shughuli ya upasuaji wa maiti ya Njoki ikisitishwa hadi Jumanne kuruhusu mamlaka ya IPOA kushiriki.