Wakazi Roka , Lamu wanalalamika kuishi kama maskwota pasi na kuwa na hatimiliki za mashamba

  • | Citizen TV
    365 views

    Zaidi ya wakaazi 7000 kutoka eneo la Roka, Sinambio katika wadi ya Hindi kaunti ya Lamu wanalalamika kuishi kama maskwota pasi na kuwa na hatimiliki za mashamba. Wanasema hali hii imesababisha mizozo ya mara kwa mara kati yao na wafugaji. Ni hali ambayo imesababisha wakaazi kuishi kwenye hofu kubwa ikizingatiwa eneo hilo limekuwa likishuhudia changamoto za usalama.