Wito wa dharura umetolewa kwa serikali ya kaunti za Elgeyo Marakwet na Baringo pamoja na serikali kuu kuingilia kati na kuharakisha juhudi za kutafuta na kuopoa mwili wa mpiga mbizi, Rodgers Kiplimo, aliyezama siku chache zilizopita katika Mto Cheploch.
Mto huo, ambao unapatikana mpakani mwa kaunti za Elgeyo Marakwet na Baringo, unajulikana kwa shughuli za upigaji mbizi ambazo huvutia watalii na wenyeji. Kiplimo anaripotiwa kuzama alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kila siku ya kupiga mbizi katika mto huo.