Mamia ya wakazi wa Cherangany, haswa wazee wamepata matibabu ya bure. Ikibainika kuwa Wengi wao hukosa huduma za afya kwa wakati unaofaa kutokana na umbali wa vituo vya afya na umaskini.
Wahudumu wa afya wanasema wazee wengi wanaugua magonjwa tofauti na hawana uwezo wa kugharamia matibabu, hali inayozorotesha afya yao. Aidha ilibainika kuwa magonjwa hayo yanaathiri wakulima wa chai na uzalishaji. Zoezi hilo la siku mbili liliandaliwa na Mamlaka ya KTDA na mashirika ya matibabu ya macho kwa lengo la kupunguza gharama ya matibabu kwa wakazi.