Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Emarti Kajiado ya Kati walalamika kuwa wametengwa

  • | Citizen TV
    130 views
    Duration: 1:38
    Wakazi wa eneo la Emarti, Kajiado ya Kati, wamelalamikia viongozi walio mamlakani wakisema wamewasahau katika miradi ya maendeleo. Wakizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kanisa la Faith Free Pentecost, wakazi hao waliomba serikali kufanikisha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, mabwawa ya maji na barabara . Aidha, waliwataka viongozi wa kaunti na kitaifa kushirikiana na wananchi kuhakikisha rasilimali za umma zinawafikia kwa usawa na kuimarisha maisha yao.