Kamishna wa Kaunti ya Embu, Maurice Wanyonyi, amewataka wakazi wa Embu kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kudhibiti ongezeko la uhalifu.
Kamishna huyo amesema kuwa operesheni zinazoendelezwa na vikosi vya pamoja tayari zimepelekea kukamatwa kwa watu wanaohusishwa na wizi wa vifaa vya kielektroniki, huku uchunguzi zaidi ukiendelea.Aidha Wanyonyi pia anasema ukosefu wa taa za barabarani ni chanzo kikuu cha uhalifu kwani maeneo yenye giza yanatumiwa na wahalifu kujificha na kutekeleza uhalifu.