Wakazi wa Jacaranda, Kilifi wadai kuhangaishwa

  • | Citizen TV
    181 views

    Wakaazi wa kaunti ndogo ya Kilifi Kaskazini eneo la Jacaranda wamelalamikia kuhangaishwa na bwenyenye anayewataka kuvamia kipande chao Cha ardhi akidai umiliki wake Wakaazi hao wanasema wameishi kwenye kipande hicho Cha ardhi Kwa zaidi ya miongo saba na wameshangazwa na hatua ya bwenyenye huyo ya kujitokeza sasa na kudai umiliki wa ardhi hiyo. Wanasema licha ya serikali kuwatambua na kuwapa stakabadhi muhimu za umiliki wa kipande hicho bwenyenye huyo amesalia kuwahangaisha kupitia maafisa wa usalama eneo hilo. Kwa sasa wanaitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati na kuwapa ulinzi sawia na kuwahakikishia umiliki wa kipande hicho cha ardhi.