Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Kapsabet wataka barabara kuu ya Kapsabet - Chavakali kukarabatiwa

  • | Citizen TV
    192 views
    Duration: 1:36
    Wakazi wa mji wa Kapsabet na maeneo jirani wanaitaka serikali kuu kufanya ukarabati wa haraka na upanuzi wa barabara kuu inayounganisha Kapsabet na Chavakali. Wakazi hao, madereva wa matatu na wahudumu wa bodaboda, wameelezea mahangaiko yao kutokana na kutelekezwa kwa barabara hiyo. Barabara hiyo imekuwa mtego wa maafa mashimo hatari yanayosababisha ajali na uharibifu wa magari. Kando na ukosefu wa ishara za barabarani, barabara hiyo pia ni nyembamba sana kiasi cha kwamba hakuna nafasi iliyotengewa wanaotembea kwa miguu au magari ya dharura. Barabara hiyo kuu inaunganisha kaunti kadhaa za eneo la magharibi.