Wakazi wa kaunti ya Kajiado wakutana na shirika la KWS kuhusu mgogoro wa wanyamapori na binadamu

  • | Citizen TV
    327 views

    Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori nchini - KWS - limefanya kikao na wakazi wanaoishi katika sehemu pana ya Amboseli, Kajiado Kusini, pamoja na wadau wengine kutafuta suluhu ya kudhibiti mgogoro baina binadamu na wanyamapori. Kikao hicho kimejiri kufuatia ongezeko la visa vya ndovu kushambulia na kuwaua wakazi na mifugo wao.