Wakazi wa kaunti ya Lamu wamefanya maandamano, wakidai ridhaa baada ya serikali kuchukua ardhi yao

  • | Citizen TV
    174 views

    Wakaazi wa kaunti ya Lamu wamefanya maandamano ya Amani wakiishinikiza serikali kuu kuwalipa ridhaa yao baada ya kuathirika na ujenzi wa mradi wa Lappset.wakaazi hao wamelalamika kuwa mashamba yao yalitwaliwa na serikali zaidi ya miaka 10 sasa kwa lengo la kuwekezwa kwenye mradi wa kawi ambao umechukua muda mrefu na kuwafanya kukosa kuendeleza kilimo kwenye mashamba yao