Wakazi wa kaunti ya Nakuru wataka eneo la Hyrax Hill kuhifadhiwa na serikali

  • | Citizen TV
    233 views

    Tuelekee katika kaunti ya Nakuru sasa ambapo, jumba la kitaifa la makumbusho ya Hyrax Hill jijini Nakuru ni kivutio cha kipekee kwa watalii wengi wanaofika kufahamu kuhusu historia ya mwanadamu wa kwanza. Kando na historia ya mwanadamu na maonyesho ya utamaduni, Hyrax Hill kama inavyofahamika na wakaazi wengi wa Nakuru vilevile huwapa watalii fursa ya kujihusisha na michezo mbalimbali . Na kama ripota wetu Maryanne Nyambura anvyoarifu sasa, nyumba hii ya makumbusho imekuwa hapa kwa zaidi ya miongo nne.