Wakazi wa kijiji cha Olpisiai, Kilgoris wataka miradi iliyokwama kukamilishwa

  • | Citizen TV
    168 views

    Wakazi wa kijiji cha Olpisiai huko Kilgoris wanaitaka serikali kukamilisha baadhi ya miradi iliyoanzishwa eneo hilo ili kuboresha miundo msingi na kufanikisha utoaji huduma. Wakizungumza katika eneo la Olpisiai, wakazi hao wanashinikiza ujenzi wa zahanati moja eneo hilo ukamilishwe wakilalamika kuwa umechukua zaidi ya miaka mitano na kuwakosesha huduma. wakazi hulazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta huduma za afya kutokana na Ukosefu wa vituo vya afya.Aidha wanataka kaunti na serikali kuu kujenga shule za kisasa eneo hilo.