Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Kilifi watakiwa kujitokeza kupata huduma za bure za matibabu ya figo kesho

  • | Citizen TV
    160 views
    Duration: 1:28
    Serikali ya Kaunti ya Kilifi imewataka wakazi kutoka Kaunti hiyo wajitokeze ili kupata huduma muhimu za Afya bila malipo. Mpango huo unalenga watu wenye magonjwa ya kudumu kama vile shinikizo la damu, ugonjwa wa sukari sambamba na ule sugu wa figo. Akihutubia wanahabari katika hospitali ya kaunti Ndogo ya Malindi kwa matayarisho ya kusherehekea siku ya figo duniani Afisa wa Afya ambaye ana utaalam wa ugonjwa wa figo Nelima Waswa amesema kuwa ipo haja ya kufanya hamasa zaidi kuhusu magonjwa sugu ili kuokoa maisha.