Shughuli za uchukuzi katika barabara kuu ya kutoka Eldoret kuelekea Malaba zilitatizwa baada ya wahudumu wa boda boda na wakazi kuandamana wakilalamikia madai ya kunyanyaswa kwa mmoja wao na afisa wa serikali ya kaunti jana jioni mjini Eldoret. Katika kaunti ya Kiambu, wakazi wa mji wa Lussigeti huko Kikuyu, walifunga barabara ya kutoka Gikambura kuelekea Kikuyu baada ya wanafunzi wawili kugongwa na gari katika barabara ya Thogoto Mutarakwa, ambapo mmoja wao alifariki huku mwingine akijeruhiwa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive