Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa maeneo ya Jwelu na Kanyasrega wanasema barabara hazipitiki

  • | Citizen TV
    118 views
    Duration: 1:58
    Wakazi wa maeneo ya Jwelu na Kanyasrega katika kaunti ndogo ya Awendo, Kaunti ya Migori, wanalalamika kuhusu hali mbaya ya barabara katika eneo hilo, wakisema hazipitiki tangu mvua ilipoanza. Wakazi hao wanasema hali mbaya ya barabara imesababisha kukatizwa kwa usafiri, huku wakazi wakipata wakati mgumu kufika kwenye maeneo yanayotoa huduma muhimu.Wakazi wanaitaka Serikali ya Kaunti ya Migori kuwajibika na kutengeneza barabara zilizoharibika huku madereva na wamiliki wa magari ya usafiri wa umma wakilalamikia hasara kubwa. Afisa Mkuu wa uchukuzi wa Kaunti hiyo, Okoth Njoga, anasema juhudi zinaendelea za kurekebisha na kutengeneza barabara kadhaa.