Wakazi wa Makueni wahamasishwa kuhusu chanjo dhidi ya Corona

  • | Citizen TV
    188 views

    Idadi ndogo ya watu wanaojitokeza kupokea chanjo ya Corona imewatia kiwewe washikadau katika sekta ya afya kaunti ya Makueni. Wizara ya afya kwenye kaunti hiyo imeanza kuwahusisha viongozi wa kidini katika kampeni ya kuwarai wakazi wa kaunti hiyo kujitokeza kwa wingi na kupata dozi zote za chanjo ya Corona.