- 190 viewsDuration: 2:12Wakazi wa Sabaki huko Magarini kaunti ya Kilifi wameitaka serikali ya kaunti hiyo kusitisha hatua ya shirika la ustawishaji kilimo ADC , ya kuwafurusha kutoka eneo wanamoishi. wakaazi hao wanasema wameishi katika kipande hicho cha ardhi kwa zaidi ya miaka 30 wakidai kuwa usimamizi wa ardhi hiyo umekuwa ukiwanyanyasa kutokana na hali yao ya uchochole. Usimamizi wa ADC ulitoa notisi ya kubomoa nyumba zao kufikia Jumatatu wiki ijayo.