Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa vijiji eneobunge Belgut wajenga daraja la muda

  • | Citizen TV
    367 views
    Duration: 2:16
    Wakazi wa vijiji vya Seretut Cheptoriet na Waldai katika eneobunge Belgut wameungana kujenga daraja la muda linalounganisha shule na soko la kijamii ili kuwaondolea wanafunzi hatari inayowakodolea macho wanapovuka mto kwenda shuleni. Awali, wanafunzi kutoka shule hizo walikuwa wakitumia gogo kama daraja ili kuvuka mto, jambo ambalo lilihatarisha maisha yao haswa wakati wa mvua. Hata hivyo, wakazi wamemkashifu Gavana wa Kericho Dkt. Erick Mutai na wawakilishi wadi wao kw akupuuza madhila yao na kuwaweka kwenye hatari ya kutumbukia mtoni na kufariki wanapovuka kuelekea kwenye shughuli za kila siku. Wakazi hao wametoa makataa kwa viongozi hao kufika eneo hilo na kushughulikia tatizo la miundombinu duni.