Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wachimbiwa visima vilivyo na mitambo ya sola ili kuendeleza miradi ya maji Pokot Magharibi

  • | Citizen TV
    386 views
    Duration: 2:06
    Chama cha maskauti nchini pamoja na VI Agroforestry miongoni mwa wadhamini wengine kimezindua miradi elfu 10 ya uchimbaji wa visima vya maji inayolenga kuhudumia watoto chini ya mradi wa ‘The Children Of the World’, Katika kaunti ya West Pokot. Akizindua mradi wa kwanza wa uchimbaji kisima katika shule ya Our Lady of Peace PSER Senior School na St. Pauls Kitelakapel eneo bunge la Kapenguria, afisa mkuu mtendaji wa chama cha maskauti Moses Tanda, alisema maji hayo yatatumiwa na nyumba elfu 10 na hasa familia maskini katika kaunti hiyo. Kwa mujibu wa msimamizi wa shirika la VI Agroforesty nchini Dorcas Munyua, mradi huo vile vile utawezesha wanafunzi kukuza mimea .