Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wahofia usalama wao baada ya mama mmoja kupigwa na kuuawa nyumbani kwake Malava

  • | Citizen TV
    3,577 views
    Duration: 1:55
    Maafisa wa polisi kutoka eneo bunge la malava kaunti ya kakamega wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya mama mmoja katika Kijiji cha Chombeli. Mwili wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 ulipatikana ndani ya nyumba yake kijijini humo. Inadaiwa kuwa watu wasiojulikana walimvamia mama huyo usiku wa Jumatatu ndani ya nyumba yake na kumpiga kwa kifaa butu katika sehemu tofauti mwilini na kisha kumwacha akiwa amefariki. Akidhibitisha kisa hicho naibu chifu wa eneo la Sasala Mike Mwonyonyo anasema ni kisa cha kushangaza akiongeza kuwa visa vya utovu wa usalama vinashuhudiwa zaidi mvua inaponyesha..