Wakazi walalamika kuwa ardhi za kukodi zinatolewa hatimiliki

  • | Citizen TV
    85 views

    Wakaazi wa Waa-Ng'ombeni katika kaunti ya Kwale wameelezea wasiwasi wao kwa kuendelea kunyakuliwa kwa ardhi za jamii zilizokamilika muda wao wa kukodishiwa. Wanasema zaidi ya ekari 6,000 za baadhi ya mashamba makubwa yaliyokua yamekodishiwa yanatolewa hati maliki upya za ukodishaji kinyume cha sheria na bila ya wakaazi na serikali ya kaunti kuhusishwa