Wakazi wazua vurugu kwenye vikao vya kutoa maoni

  • | Citizen TV
    1,351 views

    Vurugu na ghasia zilishuhudiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa katika maeneo mbali mbali ya kaunti ya tharaka nithi baada ya wakazi wenye hasira kutibua mikutano ya kujadili mswada wa bajeti wa kaunti hiyo wa mwaka huu. Wakazi wengi waliitaka serikali ya kaunti kuelezea ilivyotumia fedha za bajeti ya mwaka jana kwanza. Kulingana nao, hakuna miradi ya maendeleo yoyote katika kaunti hiyo na mikutano hiyo haitafanyika hadi serkali ya kaunti ielezee zilikokwenda zaidi ya shilingi bilioni mbili fedha za bajeti za mwaka jana wanazodai zimefujwa.