Wakenya watahitajika kuchukua upya vitambulisho

  • | KBC Video
    112 views

    Serikali imetetea kuanzishwa kwa kadi ya Maisha ili kuchukua nafasi ya vitambulisho vya zamani vya kitaifa. Kwa mujibu wa katibu anayehusika na maswala ya uhamiaji na huduma kwa raia Profesa Julius Bitok, takriban vikao 820 vya kushirikisha wananchi na wadau wengine muhimu vilifanywa katika mchakato wa kushirikisha umma, mashirika ya kijamii, viongozi wa kidini, sekta ya kibinafsi na vyombo vya habari. Bitok alisema kuwa kubadilisha ama kuchukua upya kitambulisho cha kitaifa kila baada ya miaka kumi ni mtindo wa kawaida ambao unazingatiwa na mataifa ya Uganda, Tanzania na Ufaransa. Kufikia sasa jumla ya kadi elfu 972,630 za maisha zimetolewa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive