Wakfu wa Ford wakanusha madai kuwa unafadhili maandamano

  • | Citizen TV
    629 views

    Wakfu wa Ford umejitenga na madai ya kufadhili maandamano yanayoshuhudiwa nchini Kenya. Wakijibu barua ya katibu wa Mambo ya Nje Korir Sing'oei, maafisa wa wakfu huo wameshikilia uwazi katika shughuli za wakfu huo kuhusu utoaji wa ruzuku. Haya yanajiri huku baadhi ya mashirika ya kijamii yakipinga madai kuwa yanafadhili vurugu na maandamano humu nchini. Mashirika hayo yametaja madai hayo kama njama ya kuhujumu juhudi zao za kutetea haki za kibinadamu na uwajibikaji serikalini.