Wakili Paul Gicheru afariki nyumbani kwake Karen

  • | Citizen TV
    3,635 views

    Maafisa wa upelelezi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha wakili Paul Gicheru hapa Nairobi. Wakili Gicheru ambaye atakumbukwa kwa mashtaka yaliyomkabili mbele ya mahakama ya jinai ya ICC kwa madai ya kuwahonga na kuwatishia mashahidi alifariki jana usiku. Kulingana na maafisa wa polisi na familia yake, Gicheru alifariki akiwa nyumbani kwake mtaani Karen jijini Nairobi. Kifo chake kinajiri huku mahakama hiyo ya jinai ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mashtaka dhidi yake