Wakimbiaji zaidi ya 200 washiriki mbio za Mountain to Mountain huko Nyeri

  • | Citizen TV
    282 views

    Samuel Parsoot ndiye bingwa wa mbio za Mountain to Mountain awamu ya kaunti ya Nyeri. Samuel alishinda mbio hizo kwa kukimbia kilomita 82 akitumia saa sita na dakika 50. John Githinji alishinda kitengo cha kilomita 50 huku Paul Theuri akiibuka mshindi kwenye kilomita 25. Mbio hizo zilizovutia wakimbiaji 200 zinalenga kuhifadhi mazingira na kukuza utalii Nyeri.